Skip to main content

Hebutafakari, Je, ingelikuwaje kama, umaizi bandia ingefundishwa kwa takwimuhalisia zinazopatikana na kila mtu?

Open for Good inaboresha takwimu halisia za kufundishia umaizi bandia ndani ya Afrika, Asia na kwingineko

Ukosefu wa takwimu halisi za kufundishia zenye ubora toshelevu ni mojawapo wa vikwazo vikubwa vya kurasimisha uvumbuzi wa umaizi bandia ndani ya Afrika, Asia na kwingineko. Hivyo, Open for Good inazingatia takwimuhalisia za kufundishia elimu ya umaizibandia ndani ya Afrika, Asia na kwingineko. Takwimu za kufundishia zilizo nauhalisia na zenye maswali yanayohusika ya kiufundi, ambazo mara nyingi hazizingatiwi katika mipango inayoshughulikia upatikanaji wa mifumo ya umaizibandia. Hivyo basi, Open for Good hutoa nafasiili kuratibu na kubadilisha uzoefu unaohitajika kwa sasa.

Kuongezeka upatikanaji na ubora wa takwimu za mafundishia.

Kurasimisha takwimu halisia za kufundishia umaizibandia na mifumo ya kufundishia kwa njia ya tarakishi.

Kutumia takwimu za kufundishia zilizo wakilishi na zisizo bagua.

Kurasimisha mfumo wa umaizi bandia wenye uhalisia ili kuboresha huduma za kijamii, kuimarisha maendeleo ya sekta binafsina kukuza maendeleo endelevu.

Tunayafikiaje malengo yetu?

1

Wanachama wa ushirika wanafanya takwimu za kufundishia kupatikana kwa uwazi.

Tunafanya takwimu za kufundishiazipatikane kwa uwazi, kwa kusaidia utunzaji na upatikani wa takwimu zilizopo.

2

Tunawezesha uratibu na kubadilishana uzoefu mzuri na maoni.

Tunawaleta pamoja wanajamii kujadili maendeleo ya hivi karibuni yanayohusu ukusanyaji watakwimu na matumizi ya mifumo ya umaizi bandia, tunawezesha utengenezaji waviwango pale panapohitajika na kushirikisha mifano ya mafanikio.

3

Ushirika unaongeza ufahamu kwa umma kwa manufaa ya upatikanaji wa wazi na usio na baguziwa wa takwimu za kufundishia.

Open for Good ni nini?

Ushirika wetu unakusudia kuondoa moja ya vikwazo vikubwa katika kutengenezatakwimu halisia za mifumo ya umaizi bandia : takwimu halisia za kufundishia zenye ubora toshelevu

Na ndiyo maana tumejikita kwenye takwimu halisia za mifumo ya umaizi bandia namatumizi ya elimu kwa njia mifumo ya tarakishi zilizo wazi, na bila ubaguzi. Pamojana wanachama wetu, tumedhamiria kutengeneza takwimu za kufundishia umaizi bandia.